Jumanne 26 Mei 2026 - 14:00
Wito wa Kampeni ya Kimataifa ya Kutetea Haki za Wafungwa wa Palestina

Hawza/ Makundi ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yameanzisha kampeni mpya na kuyataka makumi ya nchi kuingilia kati kuhusu hali mbaya na kuzuiliwa maelfu ya Wapalestina wasio na hatia wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Israel.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, mpango huu unaoongozwa na kundi maarufu la Red Ribbons, wanachama wa kundi la Flotilla Sumud, pamoja na mashirika ya kiraia ya Palestina, unataka kuachiliwa huru kwa zaidi ya wafungwa wa Kipalestina 9,600.

Waandaaji wa mpango huu wanasema kwamba; ni juhudi muhimu za kuzuia uhalifu wa utawala wa Kizayuni katika kipindi ambacho ripoti kuhusu unyanyasaji na ukiukwaji unaofanywa na utawala huo ndani ya mfumo wake wa mahakama zinaongezeka, miongoni mwa ukiukwaji huo ni kuwekwa kizuizini kwa utaratibu wa kifungo cha kiutawala bila kufikishwa mahakamani, mateso, pamoja na kupuuzwa kwa huduma za matibabu, aidha, wameeleza wasiwasi wao kuhusu vizuizi vya upatikanaji wa msaada wa kisheria na hali za kibinadamu ndani ya magereza.

Mpango huu umejengwa juu ya harakati za kimataifa zilizohusiana na kuzuiliwa kwa wanaharakati waliokuwa katika Msafara wa Sumud, kwa mujibu wa waandalizi, katika juhudi zilizopita zaidi ya jumbe milioni 1.2 zilitumwa kwa maafisa wa serikali katika nchi mbalimbali duniani ndani ya siku chache tu.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakieleza mara kwa mara wasiwasi kuhusu mazingira mabaya ya kuwahifadhi wafungwa hao, madai hayo yanajumuisha kuwekwa katika vizimba vya upweke, kufanyiwa unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia, pamoja na kutopatiwa huduma za matibabu zinazotosha.

Kwa sasa, wanaharakati wote wanataka kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu na kuwepo kwa uwajibikaji wa wazi zaidi kuhusu namna wafungwa hao wanavyotendewa.

Chanzo: EUPAC.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha